Kiongozi huyo aliyeiongoza Simba kwa mafanikio
makubwa amesema endapo bodi ya udhamini ya
Yanga itamkabidhi ataifanya timu hiyo kuwa zaidi
ya TP Mazembe
Aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Hassan
Dalali amesema anataka kuikodisha Yanga kwa
dau kubwa zaidi ya lile aliloahidi mwenyekiti wao
wa sasa Yusuph Manji.
Dalali ameiambia Goal , anataka kufanya hivyo
kwasababu nayeye ni mfanya biashara na
angependa kuitumia nafasi hiyo iliyowekwa wazi
na wanachama wa klabu hiyo kwasababu ana
mipango mizuri ya kutaka kuisaidia klabu hiyo
kwa kuipa kiasi kikubwa cha faida zaidi ya
asilimia 25 wanayotaka kupewa na Manji.
“Nataka kuichukua Yanga kama bodi ya
wadhamini itaridhia ombi langu na nina mipango
mizuri na klabu hii zaidi ya ile ya Manji ambayo
anataka kuwapa asilimia 25 mimi tutachukua
nusu kwa nusu,”amesema Dalali.
Kiongozi huyo aliyeiongoza Simba kwa mafanikio
makubwa amesema endapo bodi ya udhamini ya
Yanga itamkabidhi ataifanya timu hiyo kuwa zaidi
ya TP Mazembe na klabu nyingine zote kubwa
Afrika.
“Nimeamua kufanya hivyo kwa kuwa watani zetu
wenyewe wanakwenda na mambo ya kukodisha,
ninajua wana vitu vingi pale, sasa nataka
kukodisha.
Manji ametangaza kutaka kuokodisha timu ya
Yanga na nembo ya klabu kwa miaka 10 na faida
asilimia 75 kama itapatikana atachukua na 25
utachukua uongozi.
Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports
Chapisha Maoni