0

Mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe na klabu
ya Yanga Donald Ngoma ataikosa mechi ya
Jumamosi dhidi ya MO Bejaia ya Algeria.
Pambano hilo litakalopigwa katika dimba la Taifa
jijini Dar Es Salaam ni la marudiano baina ya timu
hizo katika michuano ya kombe la shirikisho
barani Afrika
Donlad Ngoma mshambuliaji Chipukizi wa Yanga
ataikosa mechi hiyo kwakua na kadi mbili za
njano akiungana pia na Geoffrey Mwashiuya
ambaye ni majeruhi pekee katika kikosi cha
Yanga.
Tayari MO Bejaia wako Dar es Salaam wakifikia
katika hoteli ya Ledger Plaza nje kidogo ya jiji la
Dar.



Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top