Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeibuka kwa
kusema kuwa ruksa kwa Mkuu wa Kitengo cha
Habari na Mwasiliano wa Yanga, Jerry Muro kukata
rufaa iwapo anahisi hakutendewa haki.
Murro amefungiwa na TFF hivi karibuni kufuatia
madai ya kulishambulia shirikisho hilo ambapo
atalazimika kutojihusisha na masuala ya soka kwa
mwaka mmoja.
Akizungumza na Championi jana, Ofisa Habari wa
TFF, Afred Lucas amefunguka kuwa, kuna taarifa
wamezipata kuwa Muro yupo mbioni kukata rufaa
na kudai kuwa kwa upande wa shirikisho hilo
halina tatizo linasubiri rufaa hiyo na watasimamia
haki.
Aidha, alieleza kuwa, madai ya kwamba bado
hajapata barua ya kusimamishwa si ya kweli na
kudai barua ambayo haijamfikia ni ya hukumu ya
kesi yake.
Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports
Chapisha Maoni