0


Ilipigwa mechi ya kumuenzi
mshambuliaji wa Uingereza, Rooney
mwenye miaka 30 ambapo yeye alicheza
kwa dakika 52 kabla ya kutolewa nje na
mchezo kusimama kwa ajili ya kupigiwa
makofi na mashabiki takribani 58,597
waliohudhuria dimbani pale.
“Usiku wa leo ni usiku ambao mimi na
familia yangu tutaukumbuka sana,”
Rooney alisema baada ya mchezo
kumalizika. Sam Allardyse ambaye ni
kocha mpya wa Uingereza alikuwepo
kwenye dimba la OT kumshuhudia
Rooney ambaye mpaka sasa amefunga
mabao 53 kwenye gemu 115 kwa taifa
lake la Uingereza!
Akipigiwa gwaride na wachezaji wa
timu hizo mbili!
Mchezaji huyu aliwekewa gwaride
maalum kuanzia karibu na eneo la
kuelekea kwenye vyumba vya
kubadilishia nguo akiwa na wanawe
watatu Kai mwenye miaka 6, Klay
mwenye miaka 3 na Rooney mdogo
mwenye umri wa miezi 7 ambao
walikuwa wamekaa mahali anapokaa Sir
Alex Ferguson ambaye ni kocha wake.
Rooney ni mchezaji wa zamani wa
Everton na amefungia United magoli 245
kwenye michezo 520 na kwa sasa
anashikilia nafasi ya pili kwa rekodi ya
ufungaji ndani ya klabu hiyo bora
duniani.
Mpaka sasa Rooney ameshinda
makombe matano ya EPL katika kipindi
chote alichokuwepo klabuni hapo, taji la
Ligi ya Mabingwa Ulaya, kombe moja la
FA, na Fifa Club World Cup. Pia, atakuwa
akijaribu kuchukua Ngao ya Jamii kwa
mara ya 4 wakati timu yake
itakapokwaana na Leicester City dimbani
Wembley Jumapili ijayo.
Baada ya mechi hiyo, Rooney
ametangaza kwamba mapato yote
yaliyotokana na mchezo huo yataenda
moja kwa moja kwa watoto na vijana
wasiojiweza nchini Uingereza, hili ni
jambo la kupongezwa sana.



Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top