0

Hatimaye
ligi kuu ya Uingereza msimu wa 2016/17 unafunguliwa leo kwa mchezo kombe la Ngao Ya
Hisani kati ya washindi wa EPL Leicester vs mabingwa wa FA Manchester United. Kuelekea mchezo huu tuangalie takwimu na rekodi mbalimbali zinazohusiana na vilabu hivi.

Takwimu na Rekodi
Mechi pekee ya Wembley baina ya United vs Leicester ilikuwa katika fainali ya FA Cup
mnamo mwaka 1963, na Manchester United
3-1.

Mechi zote za msimu uliopita za EPL baina ya vilabu hivi viwili ziliisha kwa sare ya 1-1.
Jamie Vardy alivunja rekodi ya Premier League ya kufunga katika mechi nyingi
mfululizo, rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Ruud van Nistelrooy, katika mchezo wao
kwanza vs Manchester United mnamo November 2015.

Leicester City
Hii ni mara ya kwanza Leicester City wanacheza katika Ngao ya Hisani tangu
mwaka 1971, ambapo waliwafunga Liverpool
1-0 katika uwanja wa Filbert Street. Foxers walikuwa mabingwa wa ligi daraja la pili sasa hivi Championship – msimu wa nyuma.
Mara ya mwisho Leicester mwenda Wembley
na kushinda ilikuwa katika mchezo wa fainali
ya Kombe la Ligi mnamo February 2000,
wakiwafunga Tranmere 2-1.
Katika mechi 5 zilizopita katika dimba la Wembley – wameshinda mechi 3 na kutoa
sare 2.
Hii ndio mara ya kwanza Claudio Ranieri
ataikochi timu katika dimba la Wembley.
Vardy amefunga mara 1 na kutoa assist ya
goli moja akiwa anaichezea England katika
uwanja wa Wembley.


Manchester United

Hii itakuwa mara ya 30 kwa Manchester United kucheza mchezo wa Ngao wa Hisani.
Wameshinda kikombe hiki mara 20, mara nyingi kuliko timu yoyote katika Historia ya
kikombe hicho.

United wameshinda Ngao ya hisani mara 5 kati 6 walizocheza mara ya mwisho. (2007, 2008, 2010, 2011, 2013).
Mechi zao 4 walizocheza Wembley
wameshinda zote, mechi ya mwishi kupoteza
ilikuwa fainali ya Champions League vs Barcelona 2011.
Jose Mourinho ameshindwa kushinda Ngao ya hisani mara 3 akiwa kocha wa Chelsea,
ukiwemo mchezo wa mwisho wa msimu uliopita vs Arsenal na alifungwa na United
kwa penati 2007.

Manchester United wamepoteza mechi moja
tu kati ya 15 ya Mashindano yote dhidi ya Leicester, kipigo cha magoli 5-3 mnamo
September 2014.
Zlatan Ibrahimovic amecheza mara 1 tu katika dimba la Wembley, akiwa na Sweden
ambao walifungwa 1-0 na England November 2011



Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top