0

Klabu ya Juventus ya Italia imemruhusu
mshambulizi wake Paul Pogba kufanyiwa vipimo
vya afya Old Trafford katika moja ya ishara kuwa
huenda Manchester United imeafikiana na wakala
wake kumnunua mchezaji huyo.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa
likizoni Marekani baada ya kumalizika kwa
michuano ya Euro 2016.
Pogba, 23, amekuwa akihusishwa na kuhamia Old
Trafford kwa bei ya kuvunja rekodi ya dunia ya
ununuzi wa wachezaji ya pauni milioni moja.
Pogba alichezea United mwisho dhidi ya Wolves
Machi 2012
Akiwa Old Trafford Pogba alichezeshwa katika
mechi 3 pekee.
Meneja wa United Jose Mourinho alikuwa
amedokeza kwamba klabu hiyo ilikuwa imekaribia
sana kumpata Pogba.
"Kwa sasa, Pogba ni mchezaji wa Juventus,"
amesema Allegri.
United wataanza msimu kwa mechi ya Ngao ya
Jamii dhidi ya Leicester City Jumapili.
Juventus wataanza msimu wao Serie A wiki moja
baadaye tarehe 20 Agosti.



Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top