0

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho
amesema kuwa ukosoaji uliotolewa na kocha wa
Arsenal Arsene Wenger na mwenzake wa Liverpool
Jurgen Klopp ''hauna maadili''.
Wenger na Klopp wamelalamikia uhamisho wa
pauni milioni 100 wa Paul Pogba.
''Kuna vitu ambavyo nikifanya havina maadili,lakini
wengine wakifanya ni jambo la kawaida'',alisema
Mourinho.
Mkufunzi huyo wa United ameongezea kuwa
atamsajili mchezaji mzuri wa kiungo cha kati
katika siku chache zijazo na Pogba ni muhimu.
''Kwa sasa tuna wachezaji 22,alisema.Tutakuwa na
23.Ni mchezaji wa Juve hadi pale atakapokuwa
rasmi nje''.
Soko la uhamisho linafungwa tarehe 31 mwezi
Agosti.
''Tunajaribu kila tuwezalo kufunga soko letu la
ununuzi kwa haraka iwezekanavyo''.



Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top