0

Ikiwa ni siku 5 tangu kuanza kwa Simba Week,
Klabu ya Simba leo hii imefanya usafi kwenye
mtaa wa Msimbazi yaliko makao makuu ya klabu
hiyo.
Zoezi la usafi lililohudhuriwa na mamia ya
wanachama lilianzia mzunguko wa Msimbazi hadi
kituo cha polisi Msimbazi.
Mgeni rasmi kwenye tukio hilo alikuwa Mbunge wa
Ilala Mh Mussa Azan Zungu ambaye aliisifu Simba
kwa kuwa klabu pekee kufanya shughuli za kijamii
kama kufanya usafi, kuchangia damu, kugawa
mipira, kliniki ya watoto na Simba week.
Viongozi wa Simba wakiongozwa na Makamu wa
Rais Geofrey Nyange, Katibu Mkuu Patrick
Kahemele, Msemaji wa Simba Haji Manara,
Mjumbe wa kamati ya utendaji Iddi Kajuna na
Mkurugenzi wa EAG Group Imani Kajula ambao
ndio waandaaji wa Simba week na Simba Day.
Kilele cha Simba Day ni Jumatatu ambapo Simba
itaumana na AFC Leopards.



Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top