Kamati ya Sheria na Haki za wachezaji imepisha
usajili wa wachezaji wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara huku ikiwa imepitisha jina la
Hassan Ramadhani ‘Kesi’ kuitumikia Young
Africans kuanzia msimu huu 2016/17 baada ya
kuona kuwa hana tatizo katika usajili badala yake
madai ambayo pande husika zinaweza kudaiana
wakati mchezaji anaendeleza kipaji chake.
Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Richard
Sinamtwa imepitia usajili wa timu zote na
kujiridhisha kwamba suala la mchezaji Hassan
Kessy limeegemea kwenye madai na si usajili
ambako Simba ndiye mdai kwa kumtuhumu
mchezaji huyo kuwa alianza kuitumikia Young
Africans kabla ya kumaliza mkataba wake Simba
SC. Mkataba wake ulifika mwisho, Juni 15, 2016.
Kama ni madai Simba inaweza kuendelea kumdai
Kessy au Young Africans wakati mchezaji huyo
anatumika uwanjani kwa mwajiri mpya. TFF
inafuatilia na kuangalia haki ya Simba namna ya
kupata haki yake baada ya kuwasilisha madai
kuhusu kuvunja mkataba na mwajiri wake wa
zamani.
Kanuni hazimzuii mchezaji kuendelea kucheza
kwa hoja ya madai badala yake suala hilo
linaweza kumalizwa wakati mashindano
yanaendelea. Kamati inaendelea kupitia
malalamiko na pingamizi za wachezaji wengine
na inatarajiwa kutoa taarifa rasmi kuhusu
wachezaji wote wakati wowote kuanzia sasa.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni