0

Mchezaji ghali wa Manchester United Paul Pogba
atakuwa dimbani leo baada ya kukosa mchezo
wa awali kufuatia adhabu yake ya Juventus
Manchester United baada ya kushinda 3-1 mechi
ya awali Ligi Kuu Uingereza dhidi ya
Bournemouth, Ijumaa jioni itashuka dimbani
kumenyana na Southampton.
Beki Chris Smalling pia amerejea baada ya
kufungiwa mchezo wa kwanza Ligi Kuu, na
huenda akacheza nafasi ya Daley Blind.
Nahodha wa Southampton Jose Fonte, ambaye
amekuwa akitajwa kwenye tetesi za kutimkia
Manchester United, atacheza mechi hii licha ya
kukosa mechi ya ufunguzi kwa sababu ya
kuchelewa kuanza maandalizi ya msimu.
Ryan Bertrand bado ni majeruhi hivyo Matt
Targett ataendelea kucheza kama beki wa
kushoto.
Wasemacho mameneja
Meneja wa Southampton Claude Puel
akizungumzia tetesi za Jose Fonte kuwa kwenye
rada za United: "Jose hana tatizo, ni tetesi za
ajabu tu ambazo zimekuja kabla ya mechi yetu
itakayopigwa United.
"Lakini ni mchezaji mahiri na amecheza vizuri
katika mazoezi. Jose ana uzoefu wa kutosha,
hivyo hawezi kuvurugwa na tetesi lakini
nashangaa kusikia tetesi hizi kabla ya mchezo,
siku mbili kabla ya mechi."
Takwimu muhimu
Southampton walishinda 1-0 katika kila mechi
zao mbili za mwisho walizozuru Old Trafford.
Kabla ya hapo, Saints walikwenda mwendo wa
miaka 27 mechi 19 za ligi - tangu waliposhinda
mechi yao ya mwisho ugenini dhidi ya United.
Manchester United
Mashetani Wekundu hawajafungwa nyumbani
tena tangu walipochezea kichapo kutoka kwa
Southampton Januari, mwendo wa mechi 11 za
ligi na kombe la ligi (ushindi 8, sare 3).
United wameruhusu magoli tisa tu katika uwanja
wa nyumbani msimu uliopita - rekodi bora kwa
timu zenye ushindani.
Zlatan Ibrahimovic amefunga katika mechi zake
za kwanza za ligi katika nchi nne tofauti.
Southampton
Saints wameruhusu magoli 19 ya ligi katika
mechi za ugenini msimu uliopita - timu ya pili
kwa rekodi bora nyuma ya Leicestet ambayo
iliruhusu mabao 18.
Hata hivyo, Southampton imeruhusu mabao
katika mechi 13 za Ligi Kuu mfululizo, mwendo
mrefu zaidi kucheza bila kushindwa kutoruhusu
goli tangu Novemba 2012 (walikwenda mechi
21).
Wafungaji bora msimu uliopita - Graziano Pelle
na Sadio Mane wote wameihama timu hiyo.
Kikosi kinachoweza kuanza Man United: De Gea;
Valencia, Blind, Bailly, Shaw; Fellaini, Pogba;
Martial, Rooney, Mkhitaryan; Ibrahimovic
Kikosi kinachoweza kuanza
Southampton: Forster; Cedric, Fonte, Van Dijk,
Targett; Hojbjerg, Ward-Prowse, Davis; Tadic,
Redmond, Long
Manchester United inapewa nafasi kubwa zaidi
kuibuka mshindi wa mechi hii kulingana na
ubora wa wachezaji hatari waliosheheni kikosini.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top