Simba imeanza vyema kampeni ya ligi kuu ya
Vodacom baada ya kuishushia kipigo cha mabao
3-1 Ndanda FC ya Mtwara katika mchezo
uliopigwa kwenye dimba la Taifa.
Ikicheza kwa kujiamini katika mchezo huo wa
ufunguzi, Simba iliweza kutengeneza nafasi nyingi
za kufungwa kama washambuliaji wake waliokuwa
wakiongozwa na Laurent Mavugo wangekuwa
makini, wangepachika mabao mengi.
Mavugo aliyesajiliwa kutoka Vital'O alikuwa wa
kwanza kuifungia Simba bao la kuongoza kabla
bao hilo halijasawazishwa na Omary Mponda wa
Ndanda.
Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa sare ya bao
1-1.
Kipindi cha pili Simba iliongeza mashambulizi
katika goli la Ndanda, juhudi zao zilizaa matunda
kwa kufanikiwa kupachika mabao mawili kupitia
kwa Blagnon na Kichuya.
Aidha kwenye michezo mingine ya ufunguzi wa ligi
hiyo, Mtibwa Sugar imechapwa bao 1-0 na Ruvu
Shoting, Stand United na Mbao FC zimetoka
suluhu ya 0-0.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni