Manchester City imepata ushindi wake wa pili
katika ligi kuu ya Premia baada ya kuichapa Stoke
City mabao 4-1 katika dimba la Bet365.
Manchester City imeonekana kubadilika kwa kiasi
kikubwa, mfumo huo mpya wa Guardiola umeanza
kuonyesha kila dalili ya kumpa mafanikio kocha
huyo Mhispania.
Sergio Aguero na Nolito walipachika mabao mawili
kila mmoja wakati bao pekee la Stoke lilifungwa na
Bojan kwa mkwaju wa penati.
Bao la kwanza kwa City lilifungwa na Aguero
kupitia mkwaju wa penati pia.
City imepata ushindi wa tatu katika michuano yote,
wametimiza pointi 6 kwenye EPL, wakikaa kileleni
sasa.
Aidha katika michezo hiyo mitatu Aguero
amepachika mabao 6.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni