AZAM FC imebanwa mbavu nyumbani baada ya
kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na
African Lyon katika mchezo safi na mgumu
uliomalizika usiku huu katika uwanja wa
Chamazi,Mbagala-Dar Es Salaam.
African Lyon ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata
bao mnamo dakika ya 46 baada ya mpira wa
kona uliopigwa na Hood Abdul Mayanja kwenda
moja kwa moja langoni.
Mpira ukiwa unaelekea ukingoni mashabiki
wakiwa wamekata tamaa,John Bocco
"Adebayor",aliisawazishia bao Azam FC dakika
ya 93 ya mchezo baada ya kupokea pasi safi
kutoka kwa Salum Abubakar Sure Boy na
kufanya mchezo kuisha kwa sare ya bao 1-1.
Vikosi
Azam FC:Aishi Manula,Ismail Gambo/
Mudathir Yahya,Bruce Kangwa,
Himid Mao, David Mwantika,Jean Mugiraneza,
Salum Abubakar ‘Sure Boy’/
Francesco Zekumbariwa,Shomary
Kapombe,Frank Domayo/Kipre Balou,John
Bocco na Shaaban Idd.
Afrcan Lyon;Youthe Rostand, Baraka
Jaffar,Khalfan Twenye, Hamad
Waziri, William Otone, Omar Salum, Hamad
Manzi,Mussa Nampaka, Omar
Abdallah/Abdul Hilal,Hood Mayanja na
Tito Okello.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni