0

Mshambuliaji mkongwe, Mussa Hassan Mgosi
amestaafu rasmi soka na sasa anakuwa Meneja wa
timu ya Simba SC.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba
SC, Hajji Sunday Manara amesema kwamba Mgosi
ataagwa rasmi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya
URA ya Uganda Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Pia, Manara amesema kwamba aliyekuwa Meneja
wa timu, Abbas Suleiman Ally anakuwa Mratibu wa
timu kuanzia leo na Nahodha mpya ni Jonas
Gerald Mkude.
Aidha, Manara amesema kiungo Peter Mwalyanzi
aliyesajiliwa msimu uliopita kutoka Mbeya City,
ametolewa kwa mkopo African Lyon iliyopanda Ligi
Kuu msimu huu.
"Kulingana na usajili uliofanyika msimu huu, timu
sasa itakuwa na viungo wengi na ushindani wa
namba utakuwa mkubwa, hivyo tumeona
Mwalyanzi tumpeleke African Lyon kwa mkopo
akapate nafasi ya kutunza kipaji chake"- Manara
Kikosi cha Simba SC kinaingia kambini leo Ndege
Beach Hotel, Mbweni kujiandaa na mchezo wa
kirafiki dhidi ya URA Jumapili Uwanja wa Tafa.



Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top