Kwa mujibu wa mtandao wa sokkaa.com,
wachezaji wawili bora duniani Cristiano Ronaldo
na Lionel Messi wamewaacha wengine mbali katika
kuvuta mkwanja mrefu kwa upande wa wacheza
soka.
Ronaldo, ambaye hivi karibuni ameisaidia Ureno
kushinda kombe la mataifa ya Ulaya 2026,
anaongoza chati hiyo akiwa na mshahara wa
£288,000 kwa wiki baada ya makato ya kodi (sawa
na kitita cha £15 million kwa mwaka) waka Messi
akiwa nafasi ya pili kwa kulipwa vizuri anachukua
kitita cha £275,000 (sawa na £14.5 million kwa
mwaka).
Baada ya kukamilika kwa dili lililovinja rekodi ya
uhamisho duniani la ada ya paundi milioni 89
(sawa na dola za Marekani milioni 115.98), Paul
Pogba ambaye amesaini miaka mitano kuitumikia
Manchester United mkataba wake unamfanya
alipwe £260,000 kwa wiki kabla ya kodi.
Orodha kamili kuanzia chini ya mishahara ya
wachezaji wanaolipwa pesa mingi zaidi baada ya
makato ya kodi.
David Silva £200,000
Neymar £220,000
Asamoah Gyan £227,000
Segio Aguero £240,000
Yaya Toure £240,000
Zlatan Ibrahimovic £250,000
Wayne Rooney £260,000
Paul Pogba £290,000(Kabla ya kukatwa kodi)
Lionel Messi £275,000
Cristiano Ronaldo £288,000
Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports
Chapisha Maoni