Bingwa mara nne wa medali ya dhahabu katika
michezo ya Olimpiki Mo Farah anapanga kustaafu
katika mbio za uwanjani baada ya kukamilika kwa
mashindano ya dunia mjini London,ambapo
huenda akajiunga na mbio za marathon mjini
Tokyo 2020.
Farah mwenye umri wa miaka 33 ndio
mwanaraidha aliyepata ufanisi mkubwa wa
michezo ya Olimpiki nchini Uingereza kwa
kushinda medali nyengine ya mbio za mita 5,000.
''Mwaka 2017,ningependelea kustaafu katika riadha
za uwanjani na baadaye tutaona tutakachofanya
katika marathon''.
Farah ambaye alimaliza wa nane alipokimbia mbio
za marathon kwa mara ya kwanza mjini London
miaka miwili iliopia,atakuwa na umri wa miaka 37
wakati wa michezo ya Tokyo.
''Katika mbio ndefu huwezi kujipangia kwa mda
mrefu'',alisema Farah ambaye mwenzake Galen
Rupp alijishindia medali ya shaba katika mbio za
marathon mjini Rio siku ya Jumapili.
''Lakini huwezi kusema kwamba sitoshiriki''.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni