Burudani imerejea Rasmi ndani ya uwanja wa
zamani wa Taifa maarufu kama shamba la bibi au
uwanja wa Uhuru baada ya serikali leo kupitia
kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Nape Nnauye kukabidhiwa rasmi uwanja
huo..
Nape alikabidhiwa uwanja huo leo Jumatatu toka
kwa kampuni ya Ujenzi toka China ya Beijing
Construction Engineering Group Company Limited,
(BCEG), na mshauri mwelekezi wa uwanja huo
kampuni ya kizalendo chini ya uongozi wa ke,
Injinia Aloyce Peter Mushi.
Waziri Nape aliwataka watumiaji wa uwanja huo
kulipa ada za matumizi kama inavyostahili, ili
hatimaye fedha hizo ziweze kugharimia matunzo
ya uwanja huo wenye historia kubwa kwa Taifa
letu.
Uwanja huo ambao tangu Mei 22 mwaka jana
ulishakamilika hivi sasa una uwezo wa kuchukua
mashabiki Elfu 22 na hii ni kutoka katika taarifa ya
Injinia Aloyce Peter Mushi.
Naye Meneja Mkuu wa Kampuni ya BCAG, Cheng
Long Hai, alisema, uwanja huo umewekewa
mifumo yote muhimu kama vile tangi la
kuhifadhia maji na mifumo ya maji taka, na
kuishukuru serikaliya Tanzania kwa kuiamini
kampuni yake kutekeleza mradi huo mkubwa.
Ukarabati mkubwa katika uwanja huo ulihusisha
ujenzi wa jukwaa na paa, ikiwa ni pamoja na
miundombinu mingine ya uwanja kama vile,
mifumo ya kusambaza maji, na kutoa maji taka,
uwekaji wa tanki la kuhifadhia maji, pamoja na
ujenzi wa vyoo vya kutosha uwanjani.
Baada ya Serikali kukabidhiwa Uwanja wa Uhuru
sasa mechi zote za Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara kuanzia wikiendi hii zinahama
Uwanja wa Taifa isipokua mechi kubwa ambazo
zitachezwa uwanja wa Taifa mkubwa.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni