Kiungo mpya wa Manchester United Paul Pogba
amesimamishwa kuitumikia timu yake kwa
mchezo wa kwanza wa Premier League, chama
cha soka cha England kimethibitisha.
Pogba, 23, alirejea Old Trafford kutoka Juventus
kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi ya £89.3
million, miaka 4 baada ya kuhamia klabu ya Turin
kwa ada ya £800,000 kufuatia kukosa muda wa
kucheza na mgogoro wa mkataba mpya.
Hata hivyo Pogba itambidi asubiri mpaka wiki ijayo
kucheza mchezo wake wa kwanza na klabu yake
mpya kwa sababu amefungiwa kucheza mchezo
wa Jumapili dhidi ya Bournemouth.
Kwa kujibu wa mtandao wa ShaffihDauda.Com,
Kiungo huyo wa Ufaransa amesimamishwa kwa
kosa la kupata kadi mbili za njano katika msimu
uliopita wa mashindano ya Coppa Italia, na adhabu
yake imehamia katika michezo inayosimamiwa na
Chama cha soka cha England.
Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports
Chapisha Maoni