Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF),
limemteua Noiret Jim Bacari wa Comoro kuwa
mwamuzi wa kati katika mchezo wa marudiano
utakaozikutanisha timu za taifa za vijana za
Serengeti Boys ya Tanzania na Amajimbos ya
Afrika Kusini, utakaofanyika Agosti 21, 2016
Kwenye Uwanja wa Chamazi ulioko Mbagala - nje
kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya CAF iliyofika Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) mapema wiki hii,
waamuzi wasaidizi pia wanatoka Comoro.
Waamuzi hao ambao ni washika vibendera ni
Mmadi Faissoil na Said Omar Chebli wakati mezani
atakuwa Ali Mohamed Adelaid huku Kamishna wa
mchezo huo atatoka Somalia ambaye anaitwa Amir
Abdi Hassan.
Jumamosi iliyopita, ikicheza mbele ya Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi kadhalika Naibu Balozi wa Tanzania
nchini Afrika Kusini, Rosemary Chambe Jairo, timu
ya soka ya vijana wenye umri wa chini ya miaka
17 maarufu kama Serengeti Boys ilitoka sare ya
1-1 na Afrika Kusini.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa
Dobsonville ulioko Soweto, Mji ulioko Kusini –
Magharibi mwa jiji la Johannesburg, mabao yote
yalipatikana kipindi cha pili yakiwa ni ya penalti
kwa kila upande. Afrika Kusini ndio walioanza
kupata penalti katika dakika 65 iliyofungwa na
Luke Gareth kabla ya Ally Msengi kuisawazishia
Serengeti Boys katika dakika ya 70.
Penalti ya Afrika Kusini ilitokana na mmoja wa
mabeki wa Serengeti Boys kumfanyia madhambi
Linamandla Mchilizeli wa Amajimbos ndani ya
eneo la hatari wakati ile ya Serengeti Boys
ilitoakana na beki Luke Donn wa Amajimbos
kunawa mpira eneo la hatari. Mwamuzi wa
mchezo huo alikuwa, William Koto kutoka Lesotho.
Itakumbukwa kwamba Afrika Kusini ilianza kwa
kasi dakika 10 za mwanzo wa mchezo huo,
ilipotea dakika zote 30 za kipindi cha kwanza
ambao kukosa bahati na umakini kidogo tu kwa
nyota wa Serengeti Boys kulisababisha kukosa
mabao matano yakiwamo mawili yaliyogonga
mwamba hivyo kuwatia hasira Serengeti Boys
ambao walionyesha kuwa na njaa ya mabao.
Kubanwa katika kipindi cha kwanza, kulisababisha
Kocha Mkuu wa Amajimbos kufanya mabadiliko ya
wachezaji wote watatu kipindi cha pili, wakati
Bakari Shime kwa upande wake alimpumzisha
Ibrahim na nafasi yake kuchukuliwa na Muhsin
ambaye alisaidia kuendedlea kuwabana Afrika
Kusini waliokjuwa wanawategemea nyota kama na
Mswati Mavuso na Lethabo Mazibuko.
Shukrani za pekee zinaweza kwenda kwa Kipa
Ramadhani Kabwili aliyeokoa hatari nyingi ikiwamo
mpira uliokuwa unakwenda golini uliotokana na
adhabu ndogo. Kadhalika Msengi aliyekuwa nyota
wa mchezo huo akimiliki vema idarta ya ulinzi
akishirikiaana nDickson Job.
Shime maarufu kama Mchawi Mweusi alisema:
“Nashukuru kwa matokeo . Si mabaya kwangu.
Tunarudi nyumbani kujipanga. Afrika Kusini ilikuwa
inanitia hofu ndio maana nilisema mechi itakuwa
ngumu.”
Kwa upande wake, Naibu Balozi Rosemary
alisema: “Ahsanteni vijana (Serengeti Boys) kwa
kulinda heshima yangu,” wakati Malinzi alisema:
“Sina mengi. Mkiwafunga Afrika Kusini Agosti 21,
2016 kambi inapigwa tena nje ya nchi. Sijui ni
nchi gani, lakini mtakwenda kujiandaa nje ya
nchi.”
Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports
Chapisha Maoni