Kutokana na sababu mbalimbali, Bodi ya Ligi
(TPLB) ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
imelazimika kubadili Ratiba ya Ligi Kuu kwa
michezo kadhaa ya mwanzo kama ifuatavyo.
1. Mchezo Na. 2 - Kagera Sugar vs Mbeya City
(20.08.2016)
Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 21.08.2016
katika Uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga.
Sababu ni kuwa uwanja wa Kaitaba bado utakuwa
kwenye matengenezo.
2. Mchezo Na.4 - Toto African vs Mwadui FC
(20.08.2016)
Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 24.08.2016
katika Uwanja wa CCM Kirumba. Sababu za
mabadiliko ni kuwa uwanja huo tarehe 20.08.2016
utakuwa na matumizi mengine ya kijamii.
3. Mchezo Na.13 - Kagera Sugar vs Stand United
(27.08.2016)
Mchezo huo sasa utachezwa katika Uwanja wa
CCM Kambarage. Awali timu mwenyeji wa mchezo
huo ilikuwa ni Kagera Sugar, lakini kwa sasa timu
mwenyeji atakuwa ni Stand United.
4. Mchezo Na.55 - Toto vs Ndanda (02.10.2016)
Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 03.10.2016
badala ya tarehe 02.10.2016
5. Mchezo Na.80 - Mbao FC vs Ndanda fc
(16.10.2016)
Mchezo huo umerudishwa nyuma kutoka tarehe
16.10.2016 hadi tarehe 28.09.2016. Sababu ni
kuiwezesha timu ya Ndanda kucheza michezo
miwili kwa kanda ya ziwa kwa lengo la kupunguza
gharama.
6. Mchezo Na.96 - Tanzania Prisons vs Mbao FC
(22.10.2016)
Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 23.10.2016
badala ya 22.10.2016 ili kuipa nafasi timu ya
Mbao kupumzika na kusafiri. Tayari timu za Ligi
Kuu ya Vodacom zimearifiwa na kuagizwa
kuzingatia mabadiliko hayo.
Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports
Chapisha Maoni