0

Real Madrid imeanza vyema msimu mpya wa ligi
kuu ya Hispania, La Liga Santender, baada ya
Jumapili usiku kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi
ya Real Sociedad.
Gareth Bale aliiongoza Madrid na alipachika mabao
mawili huku la tatu likifungwa na Marco Asensio.
Vijana hao wa Zidane wakicheza bila nyota wao,
Cristiano Ronaldo, walitawala mchezo huo, ushindi
ulikuwa dhahiri mikononi mwao.
Nayo Atletico Madrid imelazimishwa sare ya bao
1-1 na timu iliyopanda daraja ya Alves.
Timu hizo zilifungana kwenye dakika za majeruhi
kipindi cha pili.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top