TIMU ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya
Tanzania imejiweka katika mazingira mazuri ya
kufuzu fainali za Afrika mwakani nchini
Madagascar, baada ya jioni ya leo kuifunga
Afrika Kusini mabao 2-0 katika mchezo wa
marudiano uliochezwa katika uwanja wa Azam
Complex uliopo Chamazi,Dar Es Salaam.
Mabao yaliyoipa ushindi huo mnono Serengeti
Boys yamefungwa na Mohamed Rashid Abdallah
dakika ya 36 na Muhsin Malima Makame dakika
ya 85.Katika mchezo wa awali uliochezwa huko
Afrika Kusini wiki mbili zilizopita timu hizo
zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.
Serengeti Boys sasa itavaana na mshindi kati ya
Congo Brazaville na Namibia kabla ya
kujihakikishia kufuzu fainali za michezo ya
AFCON ya vijana mwakani nchini Madagascar.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni