0

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji
amekimbizwa hospitali baada ya kuugua
akiwa mahabusu.
Taarifa zinaeleza, Manji ambaye alikuwa
mahabusu katika kituo Kikuu cha Polisi cha
Dar es Salaam, alianza kuumwa tokea jana.
“Kweli amekimbizwa hospitali na sasa
anapatiwa matibabu,” alisema mmoja wa
watu wake wa karibu.
Manji alikuwa mahabusu ambako
amewekwa tokea Alhamisi iliyopita baada
ya kuitwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, akitajwa katika listi ya watu 65
wanaotuhumiwa katika suala la madawa ya
kulevya.
Lakini leo ameugua ghafla baada ya
kuendelea kubaki rumande kwa siku zote
licha ya kwamba hajapelekwa mahakamani.
Kumekuwa na taarifa huenda kesho
akafikishwa mahakamani, lakini bado
maofisa wa Jeshi la Polisi wamekuwa
hawataki kulizungumzia suala hilo.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top