0

Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara na wawakilishi wa klabu Bingwa Afrika Yanga
imeondolewa na Zanaco ya Zambia katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika katika mchezo
uliochezwa kwenye uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka Zambia.
Yanga wameondolewa baada ya kutoka sare ya 0-0 na Zanaco, matokeo ambayo yanaivusha
Zanaco kutokana na faida ya bao la ugenini
walilolipata katika uwanja wa taifa Dar es Salaam
juma moja lililopita walipotoka sare ya 1-1 na
Yanga.
Kwa matokeo hayo, Zanaco wanaingia kwenye
hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani
Afrika, huku Yanga wakiangukia kwenye raundi ya
tatu ya hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top