Shinikizo la kufukuzwa kocha mkongwe kabisa
aliyedumu katika klabu moja Arsene Wenger wa
Arsenal limeongezeka baada ya kuendelea kupata
matokeo mabaya.
Ikicheza ugenini Arsenal ilikubali kufungwa bao 3-1
na West Bromwich Albion katika mchezo wa
kwanza wa ligi kuu ya England.
Craig Dawson alitangulia kuipatia West Brom bao
la kwanza dakika ya ya 12 kabla ya Alexis Sanchez
hajaisawazishia Arsenal dakika 3 badae mabao
ambayo yalidumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili ndicho kilicholeta dhahama kwa
Arsenal baada ya kuruhusu kufungwa bao 2 zaidi
zikiwekwa kimiani na Hal Robson-Kanu dakika ya
55 na Craig Dawson aliyefunga bao lake la pili
katika mchezo huo dakika ya 75.
Kwa matokeo hayo Arsenal wanabaki na pointi zao
50 katika nafasi ya 5 huku West Brom wakifikisha
pointi 43 katika nafasi ya 8.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni