Azam FC
wamesema kuwa wako tayari kwa
mchezo wa nusu fainali ya michuano
ya Kombe La Shirikisho 'Azam Sports
Federation', dhidi ya Mnyama Simba
SC, utakaofanyika Jumamosi kwenye
uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa klabu ya Azam Phillip
Alando, amesema kuwa licha ya kuwa
tayari na mchezo huo lakini bado
wanaendelea na mazoezi huku morali
ya wachezaji ikiwa juu tayari kwa
mchezo huo, licha ya kukuri kuwa
mchezo huo utakuwa mgumu kwa
pande zote mbili.
-Tunaendelea na mazoezi vizuri
wachezaji wako vizuri na tunaamini
tutafanya vizuri katika mchezo huo,
tunawajua Simba ni timu nzuri wana
wachezaji wazuri na tunajua uwezo
wao kwa sababu tumecheza nao mara
nyingi na tumewasoma' Alando
alisema kwa Kujiamini.
Katika hatua nyingine Alando
ametabiri mchezo huo utakuwa wa
kuvutia kutokana na vikosi vyote
kuimarika hasa safu ya kiungo na
Ulinzi.
Mchezo wa kuvutia.
-Mchezo wa Azam na Simba utakuwa
wa kuvutia, tunatarajia upinzani mkali
kutoka pande zote na ukiangalia
michezo yetu dhidi yao ya hivi
Karibuni tumeweza kushinda Mechi
mbili kati ya nne kwa hivyo natarajia
matokeo mazuri' ameongeza Alando.
Kushiriki kimataifa.
Mchezo huo ambao utafanyika
Jumamosi utakuwa na umuhimu kwa
pande zote mbili, kwani kama mmoja
wao atatinga Fainali atakuwa
Amejihakikishia Kuliwakilisha Taifa
katika mashindano ya Shirikisho
Barani endapo hawatafanikiwa kutwaa
ubingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania
Bara.
Nusu fainali ya pili itawakutanisha
Mbao Fc na Yanga SC mchezo ambao
utafanyika Jumapili kwenye uwanja wa
CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Chapisha Maoni