Dodoma ‘DOREFA’ umelaani kitendo
kilichofanywa na Uongozi wa Klabu ya
Dar Young Africans ‘Yanga’, cha
kuwaleta wachezaji chini ya Umri wa
miaka 20 kucheza mchezo wa kirafiki
dhidi ya Combine ya Majeshi katika
kusherehesha Maazimisho ya Miaka
53 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar.
DOREFA Kupitia kwa Katibu mkuu
Hamis Kissoy imesema kitendo
kilichofanywa na Yanga si cha
kiungwana na wao kama chama
hawatokubali kuonekana kuwa
walishirikiana kufanya utapeli huo kwa
wanainchi ambao walitoa viingilio
vyao kwa ajili ya kuwaona wachezaji
Nyota wa Yanga na mambo yakawa
Tofauti.
-Sisi kama Chombo cha kusimamia
Mpira Mkoani Dodoma, tunalaani
kitendo kilichofanywa na Yanga, na
hatutaishia hapa, tunataka tuwaoneshe
wapenda soka wa mkoa huu kuwa sisi
hatukushiriki katika kuwadanganya’
Kissoy Alisema.
Yanga kulipa Fidia.
Amesema lazima wapitie makubaliano
yao kuona ni kwa namna gani Yanga
wamevunja makubaliano hayo, ili
wawabane na kuwalipa fidia kadri
wawezavyo wakazi na wapenzi wa
soka Mkoani Dodoma.
-Hatuwezi kusema lolote kwa sasa,
lazima tuyapitie upya makubaliano
yetu na tuone ni kwa namna gani
Yanga wameyavunja, lakini kama
kutakuwa na Hasara basi Yanga
watatakiwa kufidia gharama zote
ambazo zilisababishwa na wao kwa
kuvunja makubaliano ya pande zote
mbili’ Kissoy Aliongeza.
Mechi ya Kirafiki.
Ikumbukwe kwamba Yanga walishusha
kikosi B Katika mchezo wa kirafiki na
Timu ya Combine ya Majeshi, mchezo
uliomalizika kwa Sare ya 1-1, jambao
ambalo liliwakasirisha wakazi wa
Dodoma waliojitokeza kwenye uwanja
wa Jamhuri, ambapo wengi walitoka
uwanjani hata kabla ya Mchezo
kumalizika akiwemo Waziri Wa
Michezo Harrison Mwakyembe.
Chapisha Maoni