0

Bosi wa Manchester City amedokeza kuwa Gabriel Jesus na Sergio Aguero wanaweza
kucheza kwa pamoja dhidi ya Man United Alhamisi Bosi wa Manchester City Pep Guardiola ametangaza kuwa Sergio Aguero na Gabriel
Jesus watakuwepo kwenye kikosi cha Alhamisi dhidi ya Manchester United.
Aguero alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa shakani kucheza mechi hiyo baada
ya kupata majeraha madogo kwenye mechi ya nusu fainali Kombe la FA dhidi ya Arsenal, wakati Jesus akiwa hayumo dimbani tangu
Februari kuuguza majeraha.


Hata hivyo, Guardiola amedokeza kuwa wachezaji wote hao wawili watakuwa tayari kwa mechi hiyo muhimu katika mbio za kutinga nne
bora Ligi ya Uingereza.
Meneja huyo mwenye umri wa miaka 46 aliwaambia waandishi: "Gabriel Jesus yupo tayari lakini kifiziki bado hajatengemaa vema.
Sergio Aguero hali yake nzuri - atakuwa tayari.
"Aguero na Jesus wanaweza kucheza kwa pamoja, inategemea jinsi tunavyotaka kucheza.
Kama ukicheza bila ya winga, kwa namna fulani wanaweza kucheza."
City wanaingia mchezoni wakiwa na faida ya pointi moja dhidi ya United wanaoshika nafasi
ya tano katika jedwali la msimamo.


Chapisha Maoni

 
Top