0
Aliyekuwa Mkuu Wa Kitengo cha
Habari na Mawasiliano cha Klabu ya
Yanga Jerry Muro amesema
angetamani Rafiki yake Haji Manara au
yeye kurithi Kiti cha Uarais wa TFF.
Muro ameyasema hayo wakati
akihojiwa katika kipindi Cha 360 cha
Clouds TV kuhusiana na Nani
angependa awe Rais ajaye Wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini
TFF.
Amesema kwanza anakoshwa Sana na
kazi anayoifanya Rais John Pombe
Magufuli na kama ingewezakana Basi
yeye Ndiye angekuwa Rais wa TFF
Lakini Kwa sababu haliwezakani Basi
yeye au Haji Manara wanafaa
kuchukua Kiti hicho.
-Naridhishwa sana na kazi ya Rais Ya
Kutumbua majipu angeingia TFF
naamini mambo yangekuwa Poa sana
Lakini Kwa kuwa hilo haliwezakani
Basi Haji Manara au Jerry Muro
wanafaa kuwa Marais waliothibitisha
TFF" Alisema.
Kuhusu Zito Kabwe.
Aidha Muro aliulizwa kuhusiana na
namna anavyouchukulia uvumi wa
Mbunge wa Kigoma Mjini Zito Zubeiry
Kabwe kuwa miongoni mwa
wagombea urais wa TFF Alisema "Zito
Kabwe ni Mbinafsi haifai mtu Mbinafsi
kuliongoza Shirikisho kubwa Kama
Hili hapa nchini, Kabwe anapenda
Sana makuu hivyo hafai kabisa'.
Uchaguzi wa TFF.
Shirikisho la Soka nchini TFF
linatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu
Mwezi Agosti Ambapo nafasi ya Urais
imekuwa ngumu kutabirika Kwani
mbali na Jamal Malinzi Kuonesha nia
ya Kugombea Tena Lakini Bado
hawajajitokeza watu wengine waziwazi
kutangaza nia ya kuwania Kiti hicho.

Chapisha Maoni

 
Top