0
Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa Simba kufika hatua hiyo baada ya msimu uliopita kutolewa na Coastal Union hatua ya robo fainali Simba kesho Jumamosi itakuwa na kibarua
kipevu wakati itakapo wakabili Azam FC, katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Kombe la FA.

Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa Simba kufika hatua hiyo baada ya msimu uliopita kutolewa na Coastal Union hatua ya robo fainali kwa kipigo cha mabao 2-1.
Simba imetinga hatua hiyo ya nusu fainali baada ya kuwatoa Madini ya Arusha kwa bao 1-0 wakati Azam Fc yenyewe ili waondosha Ndanda FC.

Mchezo wa leo ni mtihani mkubwa kwa kocha Joseph Omog wa Simba ambaye hiyo itakuwa ni nusu fainali yake ya kwanza tangu aichukue timu hiyo kama kocha mkuu.
Shinikizo kubwa kwa Omog ni kutakiwa kuipa nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa timu hiyo hivyo ushindi mbele ya Azam ndiyo kitu pekee ambacho kinaweza kumfanya aonekane
amefanikiwa katika kibarua chake.
Omog lakini hatokuwa na mteremko kwani raia huyo wa Cameroon ana kumbukumbu mbaya ya kufungwa mwchi mbili za hivi karibuni dhidi
ya Azam FC timu ambayo aliigundisha kufukuzwa mwaka 2015.
Uwepo wa mshambuliaji Fredrick Blagnon na Laudit Mavugo kunaweza kuwa msaada kwa Omgo ambaye kwasasa anapresha kubwa ya
kuipa ubingwa wa Ligi ya Vodavom mbele ya mabingwa watetezi Yanga.
Viungo Jonas Mkude,Said Ndemla na James Kotei kunaweza kuwa msaada mkubwa kwa kocha Omog mbele ya wasambuliaji wenye njaa ya mafanikio wa Azam wakiongozwa na nahodha John Bocco na Yahya Mohamed.
Kipa Daniel Agyei raia wa Ghana anatarajiwa kurekebisha makosa yake na kutoruhusu bao kama ilivyokuwa kwenye mechi mbili zilizopita
ambazo zote alifungwa.
Kocha wa Azam Aristica Cioab naye atakuwa na kazi ya kufabya ili kuwapa matajiri wake hamasa ya kumwongeza mkataba mpya kwa kuifunga Simba na kuipeleka timu hiyo fainali
kwa mara ya pili kwake akiwa kama kocha wa Azam ni mara ya kwanza.
Mromani huyo anajivunia urejeo wa kiungo mkabaji raia wa Cameroon Joseph Kiungue pamoja na mshambuliaji wake John Bocco
ambao walikuwa majeruhi kwa muda mrefu.
Kocha huyo atakuwa anajivunia uimara wa safu yake ya kiungo inayoongozwa na Himid Mao pamoja na Salum Abubakar ambao wamekuwa
wakifanya kazi kibwa ya kuiongoza timu.
Mbali ya hao pia Cioab, atakuwa akimtwgemea zaidi kipa Aishi Manula pamoja na viunho wapembeni Joeseph Mahundi na Ramadhani
Singano .
Mcheao huo unatarajiwa kuchezwa sana eneo la kiungo kutokana na timu zote kuwa na watu wapambanaji kwenye eneo hilo hasa Azam ambayo eneo hilo lina wachezaji wengi vijana.
Mshindi katika mcheao huo anatarajiwa
kukutana na Yabga au Mbao FC mshindi wa nusu fainali ya pili utakaopigwa Jumapili jijini Mwanza.

Chapisha Maoni

 
Top