Raheem Kangezi ametoa ahadi ya
kuwapeleka wachezaji wawili wa
kikosi cha Taifa cha Vijana chini ya
umri wa miaka 17 Serengeti Boys
katika shule ya Michezo nchini
Marekani.
Kangezi amesema wanatambua
muhimu wa kulea vipaji na Ndio
Maana wamekusudia kuwapeleka
Vijana wawili katika majaribio kunako
klabu ya Seattle Sounders iliyopo
Marekani.
-Kama mnavyojua kuwa hata Mbwana
Samatta ametokea African Lyon, hivyo
sisi kama uongozi tunaona wazi
kabisa hapa kuna wakina Samatta
zaidi ya Wawili, wakirejea tu Kutoka
Gabon tutapeleka Vijana wawili katika
klabu ya Seattle Sounders inayoshiriki
ligi Kuu ya Marekani Kwa Majaribio'
Kangezi Alisema.
Kangezi aliyasema hayo wakati wa
Halfa Maalumu ya kuichangia
Serengeti Boys iliyofanyika Usiku wa
Ijumaa katika Hotel ya Serena Jijini
Dar es Salaam.
Milioni 1.
Hali kadhalika mbali na Kuwapeleka
Vijana Hao nchini Marekani, African
Lyon imechangia shilingi Milioni 1
katika mfuko wa kusaidia Maandalizi
ya Serengeti Boys kuelekea kwenye
Michuano ya Kombe la Mataifa Afrika
kwa vijana chini ya umri wa miaka 17,
zitakazofanyika kuanzia Mei 14 nchini
Gabon.
Chapisha Maoni