Majaliwa amesema kwamba
Serikali sasa imeanza
mchakato wa kutengeneza
mabilionea kupitia sekta ya
Michezo ili baadaye waje
kuisaidia nchi yao kutokana
na utajiri wao.
Waziri Mkuu ameyasema
hayo usiku wa Ijumaa katika
hoteli ya Serena, Dar es
Salaam wakati wa hafla
maalum ya kuichangia timu
ya taifa ya vijana chini ya
umri wa miaka 17, Serengeti
Boys iliyohudhuriwa na
wadau mbalimbali, akiwemo
Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo, Dk.
Harrison Mwakyembe.
“Tumejifunza vya kutosha
jinsi michezo inavyotoa
mabilionea kwenye nchi
mbalimbali duniani, ambao
wanachangia pia maendeleo
ya nchi yao kwa kiasi
kikubwa kwenye uchumi wa
nchi hizo, hivyo nasi hatuna
budi kupita njia hiyo hiyo na
sasa naamini kwamba
tumeanza, na sasa tuendelee
hivyo,”amesema Waziri
Mkuu.
Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa akizungumza wakati
wa hafla ya kuichangia
Serengeti Boys usiku wa
Ijumaa mjini Dar ea Salaam
Zaidi ya Sh. Milioni 200
zimechangwa usiku huo
katika hafla hiyo kwa ajili ya
Serengeti Boys inayotarajiwa
kushiriki Fainali za U-17
Afrika nchini Gabon Mei
mwaka huu.
Na Waziri Mkuu
akawahamasisha Watanzania
kuchangia zaidi ili kutimiza
lengo la upatikanaji wa Sh.
Bilioni 1 zisaidie ushiriki wa
timu hiyo kwenye fainali hizo
zinazotarajiwa kuanza Mei 14
hadi 28, mwaka huu nchini
Gabon.
Kwa upande wake, Waziri
Mwakyembe kama
Mwenyekiti wa Kamati ya
kuhamasisha watu kuchangia
timu hiyo, Charles Hillary
aliwapongeza waliojitokeza
kuichangia Serengeti Boys na
akaomba wengine wachangie
ili kutimiza lengo la
upatikanaji wa Sh. Bilioni 1.
Waziri Mkuu, Majaliwa
alihitimisha shughuli hiyo
kwa kwenda kupiga penalti
kumfunga mchezaji wa
kipekee kuwahi kutokea
kwenye soka ya Tanzania,
Kitwana Manara aliyeanza
kama kipa hodari miaka ya
1960 na baadaye kugeuka
kuwa mshambuliaji hatari
miaka 1970.
Rais wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
alisema timu imeandaliwa
vizuri kwa ajili ya fainali hizo
na ni matarajio yake itatimiza
dhamira ya kupata tiketi ya
kwenda kwenye fainali za
Kombe la Dunia nchini India.
Tayari Serengeti Boys ipo
mjini Younde, Cameroon
tangu jana baada ya kambi
takriban mwezi mmoja mjini
Rabat, Morocco ambako pia
ilipata mechi mbili za kirafiki
za kujipima nguvu dhidi ya
Gabon na kushinda 2-1 kila
mchezo.
Kwa ujumla Serengeti Boys
imekwishacheza mechi tano
tangu kuanza kambi rasmi ya
maandalizi fainali za Gabon,
baada ya awali kuifunga
Burundi mara mbili, Machi 30
mabao 3-0 na Aprili 1 mabao
2-0, mechi zote mbili
zikipigwa Uwanja wa Kaitaba,
Bukoba, kabla ya
kulazimishwa sare ya 2-2 na
Ghana ‘Black Starlets’ Aprili
3 Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Ikisa mjini Younde, Serengeti
Boys inatarajiwa kucheza
mechi mbili za kirafiki dhidi
ya wenyeji, Cameroon Mei 3
na 6, mwaka huu kabla ya
Mei 7 kwenda Gabon ambako
imepangwa kundi B pamoja
na timu za Mali, Niger na
Angola.
Cameroon nayo itashiriki
fainali hizo ikiwa imepangwa
Kundi A lina timu za wenyeji,
Gabon, Guinea na Ghana.
Chapisha Maoni