0
Arsene Wenger amesema timu yake ilikuwa ikimfuatilia Dele Alli, lakini ameipongeza Spurs kwa kumpa nafasi mchezaji huyo na kufamfaya
kuwa tishio Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amekiri kwamba Tottenham Hotspur inastahili kupewa
pongezi kwa kumwendeleza Dele Alli.
Kinda huyo wa miaka 21 alijiunga na Spurs akitokea MK Dons kwa paundi milioni 5 tu mnamo 2015 na amekuwa winga bora wa PFA kwa wachezaji wenye umri mdogo wa mwaka
huku akijiisimika kama mchezaji muhimu kwa klabu na timu ya taifa.
Wenger amebainisha kwamba Arsenal imekuwa ikimskauti kinda huyo mara kadhaa kipindi akiwa Milton Keynes na amesifia maendeleo ya kiungo
huyo tangu alipotua White Hart Lane.
"Tulimtazama. Alicheza Milton Keynes. Si mbali kutoka hapa. Naweza kusema amefanya vizuri mno, na ameimarika kama mchezaji kamili,"
Mfaransa huyo aliwaambia waandishi.
"Ni mchezaji hatari na anafunga mabao - Nadhani amefunga magoli 16 au 17 mwaka huu,
ni matokeo mazuri sana kwa umri wake.
Wamefanya vema kumnunua na kumpa nafasi.
Wanastahili kupongezwa kwa hilo.
Tumemwangalia mara chache; mara nyingi zaidi akiwa Milton Keynes."
Alli anatarajiwa kuanza kwenye kikosi cha Spurs watakapoikaribisha Arsenal kwenye mechi kubwa ya Kaskazini mwa London Jumapili.

Chapisha Maoni

 
Top