0
Wekundu wa Msimbazi Simba Sports
Club ‘Mnyama’ wamefanikiwa kuwa
timu ya kwanza kutinga hatua ya
Fainali ya Kombe la Shirikisho
Tanzania Bara ASFC, Baada ya
kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi
ya Azam katika mchezo wa nusu
fainali.
Katika Mchezo huo ambao umepigwa
kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es
Salaam, imeshuhudia bao pekee la
Simba likipatikana dakika ya 48 ya
Kipindi cha pili kupitia kwa Kiungo
mshambuliaji Mohamed Ibrahimi
‘MO’.
Mchezo huo ulianza kwa kasi timu
zote zikifanya mashambulizi ya
kushtukiza huku vita kubwa ikiwepo
katika eneo la kiungo lilipambwa na
Jonas Mkude, Mohamed Ibrahim na
Ibrahim Ajib kwa upande wa Simba na
Himid Mao, Salum Abubakarna
Stephen Kingue kwa upande wa
Azam.
Aidha katika dakika ya 4 tu ilimbidi
Mwamuzi wa mchezo huo Matthew
Akrama kutoa kadi ya mapema kwa
beki wa Timu ya Azam na Aggrey
Morris kwa kumchezea mchezo
usiowa kiungwana Mshambuliaji wa
Simba Shiza Kichuya, huku
Mshambuliaji wa Simba Mohamed
Ibrahim naye akipata kadi ya njano
dakika ya 5.
Kipindi cha pili timu zote zilirejea
zikiwa zimejipanga upya lakini Simba
ilionekana kufaidika zaidi na Kupata
bao katika dakika ya 48 jitihada na
bao hilo kudumu hadi mwisho wa
mchezo licha ya Azam kwa mara
kadhaa kuonekana kulishambulia
lango la Simba na Kukosa nafasi za
wazi.
Katika mchezo huo Wachezaji wawili
yaani Salum Abubakar ‘Sure Boy’
pamoja na Mfungaji wa bao la Simba
Mohamed Ibrahim walipewa kadi
nyekundu na kuzifanya timu zote
mbili kumaliza dakika 90 na wachezaji
10 kila upande.
Kwa ushindi huo Simba wanatinga
moja kwa moja katika Fainali ya
kombe hilo, wakisubiri mshindi kati ya
Mbao au Yanga ambao wanacheza
Jumapili katika nusu fainali ya pili
itakayopigwa kwenye uwanja wa CCM
Kirumba.

Chapisha Maoni

 
Top