Anthony Joshua ameonyesha kuwa yeye ndiye mfalme mpya wa ngumi za kulipwa kwa uzito wa juu baada ya kumshinda mkongwe Wladimir Klitschko kwa TKO katika raundi ya 11.
Pambano hilo la raundi 12 kwenye Uwanja wa Wembley jijini London, England lilikuwa kali na la kuvutia.
Mara kadhaa, Joshua alishambulia lakini Klitschko alionekana ni mwepesi na mjanja tofauti na mapambano mengine.
Joshua ndiye alikuwa wa kwanza kukubali kuanguka na baadaye akajibu mashambulizi na kumuangusha Klitschko.
Lakini mwamuzi kutoka Marekani
alilazimika kusimamisha pambano katika raundi ya 11 baada ya Joshua kushambulia mfululizo.
Chapisha Maoni