Tottenham Hotspurs imeendeleza kampeni yake ya “kumfukuza mwizi” kimyakimya, kwa kushinda kwa bao 1-0.
Bao hilo limefungwa na Christian Eriksen
katika ya 78 baada ya kupokea pasi safi ya Harry Kane. Huo unakuwa ushinda wa nane mfululizo kwa Tottenham ambayo inaonekana ndiyo
mpinzani namba moja wa Chelsea katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England.
Kwa ushindi wa leo, Spurs imefikisha pointi 74 na kuendeleza mbio za ubingwa dhidiI a Chelsea yenye pointi 78 huku zikiwa zimebaki mechi tano kwa kila timu.
Chapisha Maoni