(UEFA) limemtaja
mshambuliaji wa kimataifa
wa Tanzania, Mbwana Ally
Samatta kama mmoja wa
wachezaji wa kutazamwa
kwa sasa barani humo.
Katika ukurasa wake wa
Twitter, UEFA imeandika;
“Mchezaji wa kutazamwa?
Mbwana Samatta amefunga
mabao sita katika mechi zake
tano zilizopita kwa Genk,”.
Na wasifu huu unakuja
wakati Genk inajitayarisha na
mchezo wa kwanza wa Robo
Fainali ya Europa League
dhidi ya wenyeji, Celta Vigo
Alhamisi wiki ijayo Uwanja
wa Balaidos.
Tayari Nahodha huyo wa
Tanzania amekwishaweka
wazi tamaa yake kucheza
Ligi Kuu ya England na
Manchester United ni
sehemu anayotaka zaidi
kwenda.
United pia wamefuzu Nane
Bora ya Europa League na
wao Aprili 13 watakuwa
wageni wa Anderlecht
Uwanja wa Constant Vanden
Stock, Ubelgiji.
Na kwa sababu kocha wa
United, Jose Mourinho
anasaka mshambuliaji
mwenye kipaji cha kufunga,
basi Samatta anaweza
kutimiza ndoto zake iwapo
za kutua Old Trafford
atamvutia Mreno huyo.
Hadi sasa Samatta
amekwishafunga mabao 18
katika mechi 49 alizoichezea
Genk tangu asajiliwe Januari
mwaka jana akitokea TP
Mazembe ya DRC.
Kati ya mechi hizo 49,
michezo 18 Samatta alicheza
msimu uliopita na 31 msimu
huu na kati ya hiyo, ni
michezo 30 tu ndiyo alianza,
10 msimu uliopita na 20
msimu huu.
Mechi 19 kati ya hizo
alitokea benchi, nane msimu
uliopita na 11 msimu huu,
wakati 11 hakumaliza baada
ya kutolewa, tano msimu
uliopita na sita msimu huu
na katika mabao hayo 18, 12
amefunga msimu huu na sita
msimu uliopita.
Usiku huu, Samatta
anatarajiwa kuichezea Genk
katika mchezo wa kuwania
kucheza michuano ya Europa
League msimu ujao dhidi ya
wenyeji, SV Roeselare
Uwanja wa Schiervelde mjini
Roeselare.
Chapisha Maoni