0
Mlinda Mlango Bora wa Ligi Kuu Soka
Tanzania Bara Msimu uliopita Aishi
Manula ametumia Ukurasa wake wa
Instagram kukanusha taarifa za
kuhamia Kunako Timu ya Simba SC.
Manula ambaye ni kipa wa Timu ya
Soka ya Azam FC na Timu ya Taifa,
Amesema Bado ana mkataba na Azam
hadi Julai mwaka huu na hata hivyo
wapo katika mazungumzo ya
kuongeza Mkataba huo.
-Nimekuwa nikipigiwa Simu mara kwa
mara na kutumiwa Ujumbe Mfupi
'SMS' kuwa nimesain Simba SC,
Napenda kuwatoa hofu mashabiki
wa Azam FC kuwa Mimi sijasaini
mkataba na Simba' aliandika.
Azam wamenilea.
Manula aliongeza kuwa "Na siwezi
saini mkataba na timu yoyote kwani
mkataba wangu na azam unaenda
kumalizika mwezi wa Saba, Hivyo basi
niko naendelea kufanya mazungumzo
na viongozi wangu wa Azam FC kwa
ajili ya kuongeza mkataba, Pia
kisheria siruhusiwi kusaini mkataba
na timu yoyote bila mkataba wangu
wa sasa kumalizika isipokuwa
naruhusiwa kusaini na Azam pekee
kwani wao ndio waajiri wangu,
naamini mazungumzo yetu yataenda
vizuri na nitaongea mkataba katika
timu iliyonitunza na kunilea vyema
hadi leo hii" Manula Alifunguka.
Kumekuwapo Kwa Taarifa za Manula
kutakiwa na Vilabu kadhaa vikiwemo
Singida United ya Singida pamoja na
Mnyama Simba SC, na hiyo yote
inatokana na umahiri Wa mlinda
mlango huyu awapo Uwanjani.

Chapisha Maoni

 
Top