0
Mwamuzi Ahmed Kikumbo kutoka
Mkoani Dodoma amechaguliwa na
Shirikisho la Soka nchini TFF
kuchezesha Pambano la Fainali ya
Azam Sports Federation Cup Kati ya
Wekundu wa Msimbazi Simba SC na
Mbao FC 'Wagumu'.
Uamuzi huo ni Kwa mujibu wa Kanuni
ya 13 ya michuano ya Azam Sports
Federation Cup HD msimu wa
2016/17, hivyo basi Mwamuzi Ahmed
atachezesha fainali hiyo inayotarajiwa
kufanyika katika uwanja wa Jamhuri
mkoani Dodoma.
Wasaidizi.
Kikumbo atasaidiwa na Mohammed
Mkono wa Tanga na Omary Juma wa
Dodoma wakati mwamuzi wa akiba ni
Florence Zablon pia wa Dodoma
wakati Kamishna wa mchezo huo
atakuwa Peter Temu wa Arusha.
Aidha TFF imezitakia timu zote,
Simba, Mbao, Waamuzi pamoja na
Kamishna wao pamoja na wanafamilia
wa mpira wa miguu, mchezo mzuri
wenye fanaka kwa kila upande.

Chapisha Maoni

 
Top