0
Klabu ya Singida United ya Mkoani
Singida imeweka wazi kuwa Inaweza
isiwatumie wachezaji wake wa
kimataifa waliowasajili katika
michuano ya SportPesa Super Cup
itakayoanza Mwanzoni mwa Mwezi
Ujao.
Katibu Mkuu wa Klabu hiyo
Abdularhaman Sima amesema
anatambua Kiu ya Mashabiki kuwaona
wachezaji hao Lakini, Mikataba
walioyoingia nao ni Ya Awali na
kwamba bado wapo katika Vilabu vyao
wakivitumikia hadi pale
watakapokamilisha Zoezi la Usajili.
-Unajua wachezaji wote wa Kimataifa
bado wapo katika Timu zao, wengine
watakuwa na Timu za Taifa, sasa
itatupa wakati mgumu kuweza
kuwatumia katika michuano Hii
ambayo ni muda Mchache" Alisema.
Aidha Sima amewataka wapenzi wa
Singida United kuwa wavumilivu
Kwani tayari wametuma maombi ya
kuwatumia wachezaji hao Lakini
itategemea na Majibu ya wale ambao
kwa sasa wanawamiliki kuwapa
ruhusa ama laa.
-Hatujakaa Kimya hata hivyo
tumetuma maombi ya kuwatumia
Lakini Hii itategemea na Majibu ya
Vilabu wanavyovitumikia, Mfano Mzuri
ni Shafik Batambuze ambaye timu
yake ya Tusker FC itakuwa na
michezo ya Ligi Kuu Kenya hivyo ni
ngumu kumuita acheze Kwa muda
Mfupi" Aliongeza.
Watakaotumika.
Sima amesema kikosi kikubwa
kitakachotumika katika michuano hiyo
ni kile kile ambacho kimeipandisha
timu daraja pamoja na kuongezeka
kwa Kenny Ally Mwambungu ambaye
wamemsajili wiki Hii.
Wachezaji wa kimataifa wa Singida
United ni pamoja na Elisha
Muroiwa,Wisdom Mutasa, Raphael
Kutinyu, Simbarashe 'Simba' Nhivi
Sithole, pamoja na Shafik Batambuze.
Ratiba.
Aidha katika Michuano ya SportPesa
Super Cup Singida United watafungua
Dimba na Timu ya AFC Leopard,
ambapo wameshinda watakutana na
Mshindi wa mchezo wa Yanga na
Tusker FC katika Hatua ya Nusu
fainali.

Chapisha Maoni

 
Top