Winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha ametia saini
mkataba mpya wa miaka mitano ya ziada katika
klabu hiyo ya ligi ya England.
Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Ivory Coast
ameicheza timu hiyo na kufanikiwa kuifungia
mabao 34 .
Zaha, mwenye umri wa miaka 24, ameuambia mtandao wa klabu hiyo: "Palace ipo moyoni
mwangu na sidhani kwamba hadithi hii imemalizika."
Aliondoka Palace kujiunga na Manchester United mnamo 2013 kwa kitita cha pauni milioni 10 na baadaye kurudi katika klabu hiyo mnamo 2015
baada ya kuuzwa kwa mkopo London kusini.
Mwenyekiti wa klabu hiyo ya Mwewe Steve Parish ameongeza: "Wilf amekuwa akiichezea klabu hii
tangu akiwa miaka 8 na amekuwa katika kikosi cha
kwanza tangu nilipowasili katika klabu hii. Yeye
ndio bahati yetu na ni mtu ambaye hujitolea
kikamilifu daima."
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni