Je! Everton wataweza kumaliza ukame wa kutoifunga Arsenal kwao baada ya mechi 22 siku ya kufunga dimba Ligi Kuu? Ox hatacheza,
Koscielny bado mashaka
Meneja wa Arsenal amethibitisha kuwa Alex Oxlade-Chamberlain atakosa mechi ya kufunga
dimba Ligi Kuu dhidi ya Everton, na hofu imetanda juu ya uzima wa Laurent Koscielny.
Washika Mtutu hao watawakaribisha Everton wanaonolewa na Ronald Koeman katika uwanja wa Emirates Jumapili kuelekea mechi ambayo
kwao kushinda ni lazima ili kuweka hai tumaini lao kutinga nne bora.
Hata hivyo, watacheza mechi hiyo bila ya huduma ya wachezaji kadhaa muhimu katika kikosi cha kwanza, baada ya Wenger kuthibitisha kuwa Oxlade Chamberlain kwa hakika atakosa
mechi hiyo kwa sababu ya majeraha ya misuli ya paja.
Kadhalika, beki wa kati Koscielny - ambaye anasumbuliwa na tendoni naye yu shakani kwa mechi hiyo, ingawa Aaron Ramsey yu mzima
licha ya kutoka mapema katika mechi waliyoshinda dhidi ya Sunderland kwa sababu ya
majeraha ya paja.
"Oxlade-Chamberlain bado hajarejea kikosini na hatuna uhakika kama Koscielny atacheza au la!,"
Wenger aliwaambia waandishi.
"Tutamjaribu leo na kesho nitatoa maamuzi ya mwisho, Aaron Ramsey hana shida." Arsenal hawajafungwa mechi 22 za ligi na za mataji mengine dhidi ya Everton, ushindi wa mwisho kupata waToffees ugenini ulikuwa Januari
1996 katika uwanja wa Highbury.
Chapisha Maoni