0

Jose Mourinho ataendelea kutumia fedha zaidi kuisuka Man United mpya na kuirejeshea hadhi yake Ulaya, Neymar, James na Bale wakiwa kwenye orodha
Msimu wa majira ya joto hauwezi kupita bila ya James Rodriguez, Gareth Bale na Neymar kujaribu kuondoka katika klabu kubwa mbili za Hispania kutua Manchester United kucheza na Phil Jones.
Mapema juma hili, habari zimesambaa kuwa uhamisho wa Rodriguez kwenda Old Trafford
utathibitika Jumapili na kwamba Gareth Bale, kupitia wawakilishi wake ameweka bayana kuwa
anataka kuwa sehemu ya kikosi cha Jose Mourinho ikiwa ataondoka Real Madrid.
Sasa, kwa mujibu wa habari nyingine, Neymar naye anaweza kuwa kwenye mchakato wa kutua
Manchester United pia.
Akiwa amechoka kuishi chini ya kivuli cha Lionel Messi katika klabu ya Barcelona, Diario Gol
(kupitia BBC ), kimedai kuwa baba wa Mbrazili huyo amemshauri mwanaye kuondoka Camp Nou
ili aweze kujiimarisha kama mchezaji bora zaidi katika sayari hii.
United, kama inavyosemekana siku za hivi karibuni wameonyesha nia ya kumsajili. Ripoti zinadai kuwa United wanataka kumleta nyota
huyo Old Trafford kwani Jose Mourinho ataendelea kutumia fedha zaidi kuisuka Man United mpya na kuirejeshea hadhi yake Ulaya.
Ushindi wa Jumatano kwenye fainali ya Uropa
dhidi ya Ajax mjini Stockholm utakuwa mwanzo
mzuri katika harakati hizo. Na ili wampate
Neymar kufuzu kushiriki ligi ya Mabingwa ni
jambo muhimu sana kwa United.
Kutokana na ugumu walionao kumaliza nne bora,
ushindi dhidi ya klabu hiyo ya kidachi ni lazima
kwani ndiyo njia pekee kurudi kwenye michuano
ya Ulaya msimu ujao.
Ushindi pekee ndio utakaozifanya habari za kutaka kumsajili Neymar ziwe za kuaminika.


Chapisha Maoni

 
Top