Licha ya kupata jeraha lililozima ndoto zake msimu huu Zlatan Ibrahimovic amedokeza kuwa
yupo 'tayari' kwa fainali ya Uropa Man United dhidi ya Ajax
Zlatan Ibrahimovic ametania kuwa yupo 'tayari' kwa mechi ya fainali Ligi ya Europa akionyesha
maendeleo yake baada ya majeraha kwa kutembea ndani ya bwawa la kuogelea.
Licha ya kupata jeraha lililozima ndoto zake msimu huu Zlatan Ibrahimovic amedokeza kuwa
yupo 'tayari' kwa fainali Ligi ya Europa Man United dhidi ya Ajax mwezi huu.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden ameendelea kuuguza majeraha yake baada ya kufanyiwa upasuaji katika Kituo cha Afya cha
Chuo cha Pittsburgh kutibu ligamenti yake iliyodhurika.
Ibrahimovic amekuwa nje ya dimba tangu alipopata dhoruba hiyo kwenye mechi ya robo fainali robo fainali Ligi ya Europa dhidi ya
Anderlecht mwezi uliopita.
Mkongwe huyo wa miaka 35 alituma chapisho kwenye akaunti yake ya Instagram akitembea kwenye bwawa la kuogelea likiambatana na
maneno: ' Ready for the final.'
Kufuatia uhamisho huru kutoka Paris Saint- Germain msimu uliopita, Ibrahimovic amefurahia
kucheza Old Trafford.
Katika mechi 46 alizocheza United, Zlatan amefunga mabao 28 na kutoa pasi tisa za magoli
chini ya Jose Mourinho.
United wamempa ruhusa Ibrahimovic kuhudhuria kwenye mazoezi yao na kupata huduma za afya katika Carrington hata baada ya kumalizika kwa mkataba wake Juni 20.
United watarejea tena mzigoni Jumapili kukabiliana na Crystal Palace katika uwanja wa Old Trafford siku ya kufunga dimba Ligi ya Uingereza.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni