0
FAINALI ya Kombe la
Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), michuano
inayojulikana kama Azam
Sports Federation Cup (ASFC)
itafanyika Mei 28, mwaka
huu katika Uwanja
utakaotajwa baada ya droo
maalum itakayofanyika ‘Live’
Azam TV.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi
amesema jioni hii mjini Dar
es Salaam kwamba, kwa
kuwa fainali ya mwaka huu
itahusisha timu za mikoa
tofauti, Simba ya Dar e
Salaam na Mbao FC ya
Mwanza, basio itapigwa droo
maalum ya kuchagua Uwanja
wa kufanyikia mchezo huo.
Fainali ya mwaka jana
ilizikutanisha timu za Dar es
Salaam tupu, Azam na Yanga
iliyoibuka bingwa kwa
ushindi wa 3-0 hivyo
hakukuwa na droo ya
kuchagua Uwanja.
Tayari Yabga imevuliwa taji
la ASFC, kufuatia kipigo cha
1-0 kutoka kwa wenyeji,
Mbao FC katika mchezo wa
Nusu Fainali jana jioni
Uwanja wa CCM Kirumba,
Mwanza.
Yanga wenyewe walijifunga
bao hilo dakika ya 27, baada
ya beki wake, Andrew
Vincent ‘Dante’ kuunganishia
nyavuni kwake krosi ya Pius
Buswita katika harakati za
kuokoa.
Simba yenyewe iliitoa Azam
FC katika Nusu Fainali ya
kwanza Jumamosi Uwanja
wa Taifa kwa ushindi wa 1-0
pia, bao pekee la Mohammed
‘Mo’ Ibrahim kipindi cha pili,
mchezaji ambaye hata hivyo
hakumaliza mchezo baada ya
kutolewa kwa kadi nyekundu.

Chapisha Maoni

 
Top