0
Timu ya Taifa ya Soka ya Vijana ya
Tanzania Maarufu Kama Serengeti
boys imeibuka na ushindi wa Mabao
2-1 dhidi ya Timu ya Taifa ya Vijana
ya Angola katika mchezo wa Kundi B
la michuano ya Mataifa Afrika
yanayoendelea huko Nchini Gabon.
Mchezo huo umepigwa katika uwanja
wa Stade de L'Amitie uliopo Mjini
Libreville. Vijana wa Serengeti Boys
Walianza mchezo Kwa utulivu wa Hali
juu wakipigiana Pasi fupufupi na za
uhakika Huku Dimba likikamatwa
vizuri na Kiungo Assad Juma.
Ilikuwa ni dakika ya 5 baada ya
Tanzania kupiga Kona fupi iliyomkuta
Kelvin Nashon Naftali aliyeonganisha
kwa Kichwa na kumshinda Mlinda
mlango wa Angola Nsesani Emanuel
Na kutinga Wavuni.
Bao hilo halikudumu Sana Kwani
mnano dakika ya 14 mabeki wa
Tanzania walijichanganya na kuruhusu
Pedro Domingos kufunga Bao jepesi.
Baada ya Bao hilo Timu zote mbili
ziliongeza umakini zaidi na kucheza
mchezo wa kuwindana na hadi
Zinakwenda Mapumziko zilikuwa
zimelingana kwa Kila kitu Licha ya
Tanzania kuonekana kukosa nafasi
nyingi za kupata Mabao.
Dakika ya 47 ya kipindi cha pili
Yohana Mkomola akaukwamisha
mpira nyavuni lakini kibendera
akaashiria kuwa alikuwa ameotea.
Kipindi cha pili.
Tanzania walionekana wameamka
zaidi katika Mwanzo za kipindi cha pili
Ambapo katika ya 56 Abdul Suleiman
alipiga shuti kali Lakini likapanguliwa
na kipa wa Angola na kuwa kona
tasa.
Kosa kosa ziliendelea kwa vijana wa
Serengeti Boys Lakini ilipotimu dakika
ya 67 shambulizi La kushtukiza
lilimfikia Yohana Mkomola ambaye
alitoa Pasi Murua kwa Abdul Hamis
Suleiman ambaye bila ajizi
akaukwamisha Mpira Wavuni na
kuiandikia Tanzania bao la Pili.
Dakika ya 74 Amanusra Tanzania
waandike bao la tatu Lakini kukosa
umakini kwa Mshambualiaji Yohana
Mkomola ikawa ahueni kwa Angola.
Hadi filimbi ya kumaliza mchezo
Tanzania wakatoka kifua mbele kwa
kuwatandika Angola kwa mabao 2-1.
Msimamo Kundi B.
Ushindi huo unawafanya Serengeti
Boys kukusanya Alama 4 na kukwea
hadi Kileleni mwa Kundi B Huku
wakisubiri mchezo kati ya Niger na
Mali ambao Utaanza saa 2:30 usiku.

Chapisha Maoni

 
Top