Flugence Novatus amesema timu hiyo
haijapoteza matumaini ya kubaki Ligi
Kuu msimu ujao na kuwataka
wanayoiombea timu hiyo kusubiri
mchezo wa mwisho na kuona uwezo
wao.
Novatus ambaye Timu yake ilipoteza
mchezo muhimu dhidi ya Yanga
Jumanne amewatoa hofu mashabiki
na wapenzi wa Toto Africans na
kuwaahidi kuwa wataendele kuiona
Ligi Kuu timu hiyo msimu ujao.
Asilimia 100
-Tulipoteza mchezo muhimu dhidi ya
Yanga haijalishi bado tuna nafasi ya
kubaki Ligi Kuu tuna mchezo mmoja,
tumebakiwa na mchezo dhidi ya
Mtibwa Sugar tutajitahidi tutashinda
na tutabaki Ligi Kuu”, amesema
Novatus.
Kocha huyo ambaye aliahidi kushinda
Mechi nne kati ya saba amesema
kuwa licha ya Timu hiyo kupata
matokeo mabaya Lakini ameisaidia
kuinua kiwango chao tangu
alipojiunga nao na kuwa morali ya
wachezaji uwanjani imerejea.
Nafasi ya 15
Toto Africans wapo katika nafasi ya 15
wakiwa na alama 29, watahitaji
kushinda mchezo wa mwisho wa Ligi
hiyo dhidi ya ‘Wakata Miwa’ Mtibwa
Sugar katika mchezo ambao
utafanyika kwenye uwanja wa
Manungu Complex Mkoani Morogoro
Mei 20 mwaka huu.

Chapisha Maoni