0
Kuanzia msimu ujao, wachezaji wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza wenye mazoea ya kusaka penalti au mkwaju wa ikabu kupitia udanganyifu watachukuliwa hatua.
Kwenye sheria mpya zilizopitishwa na bodi ya usimamizi leo katika mkutano wake wa kila mwaka, kamati maalum itatathmini video za mecho za wikendi kila jumatatu kuangalia visa vya
udanganyifu.
Kamati hiyo itawajumuisha mmoja wa wasimamizw wa mechi, meneja wa zamani na mchezaji wa zamani.

Mchezaji atakayepatikana kujirusha akisaka penalti, kupelekea utoaji wa kadi nyekundu au njano, ataadhibiwa kwa kupigwa marufuku na kukosa
baadhi za mechi. Shirikisho la soka nchini Uingereza FA, limefafanua
kuwa madhambi hayo yatajulikana kama ''utapelw wa msimamizi wa mechi''.
Mabadiliko hayo mapya yalihitaji uungwaji mkono kutoka ligi kuu ya Premier nchini Uingereza, ligi ya
daraja la chini, EFL na muungano wa wachezaji, PFA.
Wakati huo huo, FA imepitisha mabadiliko zaidi yakiwemo kutenga nafasi tatu kwa wanawake ifikapo 2018, kupuguza wanachama wa bodi hadi
10 na kuwashirikisha waanachama kumi na moja zaidi kuonyesha usawa.

Chapisha Maoni

 
Top