Étienne Ndairagije amesema kuwa
wako tayari kwa mchezo dhidi ya
Yanga utakaofanyika Jumamosi
kwenye uwanja wa CCM
Kirumba,Mwanza na kuwa alama tatu
muhimu ni zao.
Akizungumza na mtandao huu
Ndairagije amekiri ni mchezo utakuwa
mgumu kwa kuwa timu zote zinahitaji
kushinda kwa maslahi tofauti Mbao
akipambana kubaki Ligi Kuu msimu
ujao wakati Yanga wakihitaji kumaliza
Ligi wakiwa anaongoza kwa pointi na
magoli.
Timu zote zimejiandaa
-Tumefanya maandalizi ya kutosha
tunafahamu ugumu wa mchezo huo
tumejiandaa tunahitaji pointi tatu ili
kubaki Ligi Kuu msimu ujao, Tunajua
Yanga ni timu nzuri na hao pia
wamekuwa wakifanya mazoezi lakini
sisi tuko tayari mpira ni maandalizi
",amesema kocha huyo.
Mapungufu
Kuhusu mwenendo wa Timu hiyo
kupoteza michezo miwili mfululizo
Ndairagije amesema hayo yamepita
waliyaona makosa yao na tayari
wameyafanyia kazi.
-Tumeyasahau yaliyopita makosa
ambayo tuliyafanya Kagera
tuliyafanyia kazi na sasa focus iko
kwa mchezo wetu dhidi ya Yanga
ambao ni lazima tushinde,
hatujajipanga kupoteza tumejipanga
kushinda.
Mashabiki
Kocha huyo amewapatia matumaini
mashabiki wa Mbao Fc na kuwaomba
kujitokeza kwa wingi ili kuishangilia
timu hiyo ambapo amewaahidi
kutarajia burudani ya aina yake.
- Niwashukuru Mashabiki wetu kwa
kuendelea kutuunga mkono ata wakati
mambo ni magumu nawaomba
wajitokeze Jumamosi kwenye mchezo
wetu dhidi ya Yanga waone soka safi
vijana wao wataonyesha, amesema
kocha huyo raia wa Burundi.
Mbao Fc walio katika nafasi ya 13
wakiwa na alama 30 wanahitaji
ushindi katika mchezo huo wa
mwisho ili kuongeza matumaini ya
kubaki Ligi kuu msimu ujao.

Chapisha Maoni