iliyoanza safari yake Jumamosi ya Agosti 20 mwaka jana, inatia nanga leo
Mei 20, 2017.
Mechi saba zitachezwa
kwenye viwanja tofauti –
kuanzia Taifa, Dar es Salaam
ambako Simba SC watakuwa
wenyeji wa Mwadui FC ya
Shinyanga na CCM Kirumba
mjini Mwanza,
ambako mabingwa watetezi,
Yanga watakuwa wageni wa
Mbao FC.
Mechi nyingine ni kati ya
Azam na Kagera Sugar
Uwanja wa Azam Complex,
Chamazi, Dar es Salaam, Maji
Maji na Mbeya City Uwanja
wa Maji Maji, Songea, Stand
United na Ruvu Shooting
Uwanja wa Kambarage,
Shinyanga, Mtibwa Sugar na
Toto Africans Uwanja wa
Manungu, Turiani, Morogoro,
Tanzania Prisons na African
Lyon Uwanja wa Sokoine,
Mbeya na Ndanda FC na JKT
Ruvu Uwanja wa Nangwanda
Sijaona, Mtwara.
Yanga inaongoza Ligi Kuu
kwa pointi zake 68, ikifuatiwa
na Simba yenye pointi 65,
Azam FC 52, Kagera Sugar
50, Mtibwa Sugar 41, Ruvu
Shooting 36, Stand United
35, sawa na Mwadui,
Tanzania Prisons 34, Mbeya
City 33, Maji Maji 32, African
Lyon 31, Mbao FC 30, sawa
na Ndanda FC, Toto African
29 na JKT Ruvu 23 baada ya
kila timu kucheza mechi 29.
Abiria wapya watatu wa MV
Ligi Kuu, Singida United,
Njombe Mji na Lipuli ya
Iringa tayari wapo kwenye
mlango wa kupandia meli
hiyo na tiketi zao, wakati JKT
Ruvu tayari safari yake
imefikia tamati na baada ya
mechi za leo timu mbili
nyingine za kuteremka
zitajulikana.
Toto, Mbao, Ndanda, Maji
Maji na African Lyon kati ya
hizo kuna timu mbili za
kuungana na JKT Ruvu – na
hilo litajulikana baada ya
mechi za leo jioni.
Yanga wamekwishaanza
kushangilia ubingwa tangu
baada ya mchezo dhidi ya
Toto Africans wakishinda
1-0, lakini ili wawe na amani,
wanatakiwa kushinda
mchezo wa leo dhidi ya
Mbao FC, ili kuwafunga
mdomo mahasimu wao,
Simba SC ambao wametishia
kukata rufaa FIFA kutaka
warudishiwe pointi tatu za
mezani za Kagera Sugar.
Simba wanaamini wakishinda
kesho na Yanga wakafungwa
na Mbao, wanaweza kutimiza
ndoto za ubingwa kama
watashinda na rufaa yao
FIFA.
Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) limepeleka Kombe la
mfano kwenye Uwanja wa
Taifa na Kombe halisi Uwanja
wa CCM Kirumba ili kati ya
Simba na Yanga timu moja
ikabidhiwe taji ikishinda
ubingwa wa ligi.
Sahau kuhusu mchuano wa
ubingwa na vita ya kuepuka
kushuka Daraja, uhondo
mwingine katika mechi za
leo za kufunga msimu ni
kinyang’anyiro cha ufungaji
bora wa Ligi Kuu,
kikiwahusisha Simon Msuva
wa Yanga mabao 14,
Abdulrahman Mussa wa Ruvu
Shooting mabao 13 na
Mbaraka Yussuf wa Kagera
Sugar mabao 13.
Wakati MV Ligi Kuu
inakwenda kutia nanga leo
jioni, maswali ni matatu, nani
wa kuizuia Yanga kutetea
ubingwa, nani mfungaji bora
na timu zipi zinashuka?

Chapisha Maoni